Native Bible

Exodus 9:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana akaweka wakati na kusema, “Kesho Bwana atalitenda hili katika nchi.”

Exodus 9:5 in English

Exodus 9:5 · Berean Standard Bible

The LORD set a time, saying, “Tomorrow the LORD will do this in the land.”

Context

3mkono wa Bwana utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ngʼombe wako, kondoo na mbuzi. 4Lakini Bwana ataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’ ” 5Bwana akaweka wakati na kusema, “Kesho Bwana atalitenda hili katika nchi.” 6Siku iliyofuata Bwana akalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa wana wa Israeli aliyekufa. 7Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.