Kutoka 9:17
Exodus 9:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bado unaendelea kujiinua juu ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende.
Exodus 9:17 in English
Exodus 9:17 · Berean Standard Bible
Still, you lord it over My people and do not allow them to go.
Context
15Kwa kuwa mpaka sasa ningelikuwa nimenyoosha mkono wangu na kukupiga wewe na watu wako kwa pigo ambalo lingekufutilia mbali juu ya nchi. 16Lakini nimekuinua wewe kwa kusudi hili hasa, ili nipate kukuonyesha uwezo wangu, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote. 17Bado unaendelea kujiinua juu ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende. 18Kwa hiyo, kesho wakati kama huu nitaleta mvua mbaya sana ya mawe ambayo haijapata kunyesha katika nchi ya Misri, tangu siku ilipoumbwa mpaka leo. 19Sasa toa amri urudishe wanyama wote watoke malishoni na chochote ambacho kipo mashambani waje mpaka mahali pa usalama, kwa sababu mvua ya mawe itanyesha juu ya kila mtu na kila mnyama ambaye hajaletwa ndani ambao bado wako nje mashambani, nao watakufa.’ ”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.