Kutoka 7:8
Exodus 7:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana akamwambia Mose na Aroni,
Exodus 7:8 in English
Exodus 7:8 · Berean Standard Bible
The LORD said to Moses and Aaron,
Context
6Mose na Aroni wakafanya sawasawa kama vile Bwana alivyowaagiza. 7Mose alikuwa na umri wa miaka themanini na Aroni alikuwa na umri wa miaka themanini na mitatu walipozungumza na Farao. 8Bwana akamwambia Mose na Aroni, 9“Farao atakapowaambia, ‘Fanyeni muujiza,’ basi mwambie Aroni, ‘Chukua fimbo yako na uitupe chini mbele ya Farao,’ nayo fimbo itakuwa nyoka.” 10Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile Bwana alivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.