Kutoka 5:20
Exodus 5:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walipoondoka kwa Farao, wakawakuta Mose na Aroni wakingojea kukutana nao,
Exodus 5:20 in English
Exodus 5:20 · Berean Standard Bible
When they left Pharaoh, they confronted Moses and Aaron, who stood waiting to meet them.
Context
18Sasa nendeni kazini. Hamtapewa nyasi zozote, nanyi ni lazima mtengeneze matofali.” 19Wasimamizi wa Kiisraeli walitambua kuwa wako taabani walipoambiwa, “Hamtakiwi kupunguza idadi ya matofali mliotakiwa kutengeneza kila siku.” 20Walipoondoka kwa Farao, wakawakuta Mose na Aroni wakingojea kukutana nao, 21wakawaambia Mose na Aroni, “Bwana na awaangalie awahukumu ninyi! Mmetufanya tunuke kwa Farao na maafisa wake, nanyi mmeweka upanga mikononi mwao ili kutuua sisi.” 22Mose akarudi kwa Bwana na kumwambia, “Ee Bwana, mbona umewaletea watu hawa taabu? Kwa nini basi ukanituma mimi?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.