Native Bible

Exodus 37:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne.

Exodus 37:13 in English

Exodus 37:13 · Berean Standard Bible

He cast four gold rings for the table and fastened them to the four corners at its four legs.

Context

11Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 12Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,* na kuufanyia ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. 13Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 14Pete hizo ziliwekwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. 15Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.