Kutoka 36:21
Exodus 36:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi,* na upana wa dhiraa moja na nusu,*
Exodus 36:21 in English
Exodus 36:21 · Berean Standard Bible
Each frame was ten cubits long and a cubit and a half wide.*
Context
19Kisha wakatengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.* 20Wakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 21Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi,* na upana wa dhiraa moja na nusu,* 22zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. 23Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.