Kutoka 36:15
Exodus 36:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mapazia hayo kumi na moja yalikuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,* na upana wa dhiraa nne.
Exodus 36:15 in English
Exodus 36:15 · Berean Standard Bible
Each of the eleven curtains was the same size—thirty cubits long and four cubits wide.*
Context
13Kisha wakatengeneza vifungo hamsini vya dhahabu, na wakavitumia kufunga na kuunganisha zile fungu mbili za mapazia pamoja ili maskani ipate kuwa kitu kimoja. 14Wakatengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. 15Mapazia hayo kumi na moja yalikuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,* na upana wa dhiraa nne. 16Wakaunganisha mapazia matano kuwa fungu moja, na hayo mengine sita kuwa fungu lingine. 17Kisha wakatengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.