Kutoka 35:26
Exodus 35:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wanawake wote waliopenda na waliokuwa na ujuzi wakasokota singa za mbuzi.
Exodus 35:26 in English
Exodus 35:26 · Berean Standard Bible
And all the skilled women whose hearts were stirred spun the goat hair.
Context
24Wale waliotoa sadaka ya fedha au shaba wakavileta kama sadaka kwa Bwana, na kila aliyekuwa na mti wa mshita kwa ajili ya kazi yoyote ile akauleta. 25Kila mwanamke aliyekuwa na ujuzi alisokota kwa mikono yake na alileta kile alichosokota, iwe ni nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi. 26Wanawake wote waliopenda na waliokuwa na ujuzi wakasokota singa za mbuzi. 27Viongozi wakaleta vito vya shohamu pamoja na vito vingine vya thamani kwa ajili ya kuweka kwenye kisibau na kwenye kifuko cha kifuani. 28Wakaleta pia vikolezi na mafuta ya zeituni kwa ajili ya mwanga, kwa ajili ya mafuta ya upako na kwa ajili ya uvumba wenye harufu nzuri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.