Kutoka 34:31
Exodus 34:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Mose akawaita, kwa hiyo Aroni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao.
Exodus 34:31 in English
Exodus 34:31 · Berean Standard Bible
But Moses called out to them; so Aaron and all the leaders of the congregation returned to him, and Moses spoke to them.
Context
29Mose alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa ukingʼaa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Bwana. 30Aroni na Waisraeli wote walipomwona Mose, kuwa uso wake unangʼaa, waliogopa kumkaribia. 31Lakini Mose akawaita, kwa hiyo Aroni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao. 32Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Bwana alizompa katika Mlima wa Sinai. 33Mose alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.