Kutoka 32:28
Exodus 32:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walawi wakafanya kama Mose alivyoamuru, siku ile wakafa watu wapatao 3,000.
Exodus 32:28 in English
Exodus 32:28 · Berean Standard Bible
The Levites did as Moses commanded, and that day about three thousand of the people fell dead.
Context
26Kwa hiyo Mose akasimama kwenye ingilio la kambi, akasema, “Yeyote aliye upande wa Bwana, aje upande wangu.” Walawi wote wakamjia. 27Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ” 28Walawi wakafanya kama Mose alivyoamuru, siku ile wakafa watu wapatao 3,000. 29Kisha Mose akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa Bwana, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.” 30Siku iliyofuata Mose akawaambia watu, “Mmefanya dhambi kubwa. Lakini sasa nitapanda juu kwa Bwana, labda nitaweza kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.