Kutoka 28:2
Exodus 28:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mshonee Aroni ndugu yako mavazi matakatifu ili yampe ukuu na heshima.
Exodus 28:2 in English
Exodus 28:2 · Berean Standard Bible
Make holy garments for your brother Aaron, to give him glory and splendor.
Context
1“Mtwae Aroni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. 2Mshonee Aroni ndugu yako mavazi matakatifu ili yampe ukuu na heshima. 3Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Aroni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani. 4Haya ndiyo mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kisibau, kanzu, joho lililorembwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Aroni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.