Kutoka 28:14
Exodus 28:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo.
Exodus 28:14 in English
Exodus 28:14 · Berean Standard Bible
and two chains of pure gold, made of braided cord work; and attach these chains to the settings.
Context
12na uvifungie juu ya vipande vya mabega ya kisibau yawe kama vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli. Aroni atavaa majina hayo mabegani mwake kama kumbukumbu mbele za Bwana. 13Tengeneza vijalizo vya dhahabu 14na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo. 15“Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. 16Kitakuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja* na upana wa shibiri moja, na kikunjwe mara mbili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.