Native Bible

Exodus 27:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba.

Exodus 27:2 in English

Exodus 27:2 · Berean Standard Bible

Make a horn on each of its four corners, so that the horns are of one piece, and overlay it with bronze.

Context

1“Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu;* itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano,* na upana wake dhiraa tano. 2Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba. 3Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto. 4Kisha tengenezea hayo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila moja ya hizo pembe nne za huo wavu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.