Kutoka 25:26
Exodus 25:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne.
Exodus 25:26 in English
Exodus 25:26 · Berean Standard Bible
Make four gold rings for the table and fasten them to the four corners at its four legs.
Context
24Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 25Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,* na ufanyie ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. 26Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 27Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko itakayotumika kuibebea hiyo meza. 28Tengeneza mipiko hiyo kwa mbao za mshita, uifunike na dhahabu, uitumie kubeba hiyo meza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.