Native Bible

Exodus 25:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli.

Exodus 25:22 in English

Exodus 25:22 · Berean Standard Bible

And I will meet with you there above the mercy seat, between the two cherubim that are over the ark of the Testimony;* I will speak with you about all that I command you regarding the Israelites.

Context

20Makerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, yakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko. 21Weka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku. 22Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli. 23“Tengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,* upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu. 24Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.