Kutoka 23:10
Exodus 23:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao,
Exodus 23:10 in English
Exodus 23:10 · Berean Standard Bible
For six years you are to sow your land and gather its produce,
Context
8“Usipokee rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha wale waonao, na kupinda maneno ya wenye haki. 9“Usimwonee mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri. 10“Kwa muda wa miaka sita mtapanda mashamba yenu na kuvuna mazao, 11lakini katika mwaka wa saba usiilime ardhi wala kuitumia, ili watu walio maskini miongoni mwenu waweze kupata chakula kutoka kwenye hayo mashamba, nao wanyama pori wapate chakula kwa yale mabaki watakayobakiza. Utafanya hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni. 12“Kwa siku sita fanya kazi zako, lakini siku ya saba usifanye kazi, ili maksai wako na punda wako wapate kupumzika, naye mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwako, pamoja na mgeni, wapate kustarehe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.