Native Bible

Exodus 2:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mose akatazama huku na huko asione mtu yeyote, akamuua yule Mmisri, akamficha mchangani.

Exodus 2:12 in English

Exodus 2:12 · Berean Standard Bible

After looking this way and that and seeing no one, he struck down the Egyptian and hid his body in the sand.

Context

10Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina lake Mose akisema, “Nilimtoa kwenye maji.” 11Siku moja, baada ya Mose kukua, akaondoka kwenda walikokuwa watu wake, na akachunguza jinsi walivyokuwa wakifanya kazi ngumu. Akamwona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmojawapo wa watu wake. 12Mose akatazama huku na huko asione mtu yeyote, akamuua yule Mmisri, akamficha mchangani. 13Kesho yake akatoka, akaona Waebrania wawili wakipigana. Akamuuliza yule aliyekosa, “Mbona unampiga Mwebrania mwenzako?” 14Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Ndipo Mose akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.