Kutoka 2:10
Exodus 2:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina lake Mose akisema, “Nilimtoa kwenye maji.”
Exodus 2:10 in English
Exodus 2:10 · Berean Standard Bible
When the child had grown older, she brought him to Pharaoh’s daughter, and he became her son. She named him Moses * and explained, “I drew him out of the water.”
Context
8Binti Farao akamjibu, “Ndiyo, nenda.” Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. 9Binti Farao akamwambia, “Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa.” Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea. 10Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina lake Mose akisema, “Nilimtoa kwenye maji.” 11Siku moja, baada ya Mose kukua, akaondoka kwenda walikokuwa watu wake, na akachunguza jinsi walivyokuwa wakifanya kazi ngumu. Akamwona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmojawapo wa watu wake. 12Mose akatazama huku na huko asione mtu yeyote, akamuua yule Mmisri, akamficha mchangani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.