Kutoka 18:24
Exodus 18:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mose akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema.
Exodus 18:24 in English
Exodus 18:24 · Berean Standard Bible
Moses listened to his father-in-law and did everything he said.
Context
22Waweke wawe waamuzi wa watu kwa wakati wote, lakini waambie wakuletee kila shauri lililo gumu; yale yaliyo rahisi wayaamue wao wenyewe. Hii itafanya mzigo wako kuwa mwepesi, kwa sababu watashirikiana nawe. 23Kama ukifanya hivi, na ikiwa Mungu ameagiza hivyo, utaweza kushinda uchovu, nao watu hawa wote watarudi nyumbani wameridhika.” 24Mose akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema. 25Mose akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. 26Wakatumika kama waamuzi wa watu kwa wakati wote. Mashauri magumu wakayaleta kwa Mose, lakini yale yaliyo rahisi wakayaamua wenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.