Native Bible

Exodus 17:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa hiyo Yoshua akalishinda jeshi la Waamaleki kwa upanga.

Exodus 17:13 in English

Exodus 17:13 · Berean Standard Bible

So Joshua overwhelmed Amalek and his army with the sword.

Context

11Ikawa wakati wote Mose alipokuwa amenyanyua mikono yake, Waisraeli walikuwa wakishinda, lakini kila aliposhusha mikono yake Waamaleki walishinda. 12Mikono ya Mose ilipochoka, wakachukua jiwe na kumpa alikalie. Aroni na Huri wakaishikilia juu mikono ya Mose, mmoja upande huu na mwingine upande huu. Wakaitegemeza mikono yake ikabaki thabiti mpaka jua lilipozama. 13Kwa hiyo Yoshua akalishinda jeshi la Waamaleki kwa upanga. 14Kisha Bwana akamwambia Mose, “Andika mambo haya katika kitabu ili yakumbukwe, na uhakikishe kwamba Yoshua amesikia, kwa sababu nitafuta kabisa kumbukumbu la Amaleki chini ya mbingu.” 15Mose akajenga madhabahu na kuiita Yehova Nisi.*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.