Kutoka 15:10
Exodus 15:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini ulipuliza kwa pumzi yako, bahari ikawafunika. Wakazama kama risasi kwenye maji makuu.
Exodus 15:10 in English
Exodus 15:10 · Berean Standard Bible
But You blew with Your breath, and the sea covered them. They sank like lead in the mighty waters.
Context
8Kwa pumzi ya pua zako
maji yalijilundika.
Mawimbi ya maji yakasimama imara kama ukuta,
vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari. 9“Adui alijivuna,
‘Nitawafuatia, nitawapata.
Nitagawanya nyara;
nitajishibisha kwa wao.
Nitafuta upanga wangu
na mkono wangu utawaangamiza.’ 10Lakini ulipuliza kwa pumzi yako,
bahari ikawafunika.
Wakazama kama risasi
kwenye maji makuu. 11“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama wewe, Ee Bwana?
Ni nani kama Wewe:
uliyetukuka katika utakatifu,
utishaye katika utukufu,
ukitenda maajabu? 12Uliunyoosha mkono wako wa kuume
na nchi ikawameza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.