Kutoka 14:6
Exodus 14:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo akaandaliwa gari lake la vita, naye akaenda pamoja na jeshi lake.
Exodus 14:6 in English
Exodus 14:6 · Berean Standard Bible
So Pharaoh prepared his chariot and took his army with him.
Context
4Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi Bwana.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo. 5Mfalme wa Misri alipoambiwa kuwa Waisraeli wamekimbia, Farao na maafisa wake wakabadili nia zao kuhusu Waisraeli, wakasema, “Tumefanya nini? Tumewaachia Waisraeli waende zao na tumeukosa utumishi wao!” 6Kwa hiyo akaandaliwa gari lake la vita, naye akaenda pamoja na jeshi lake. 7Akachukua magari bora mia sita, pamoja na magari mengine yote ya Misri, pamoja na maafisa wa magari hayo yote. 8Bwana akaufanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, kwa hiyo akawafuatia Waisraeli, waliokuwa wakiondoka Misri kwa ujasiri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.