Esta 5:7
Esther 5:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Esta akajibu, “Haja yangu na ombi langu ni hili:
Esther 5:7 in English
Esther 5:7 · Berean Standard Bible
Esther replied, “This is my petition and my request:
Context
5Mfalme akasema, “Mleteni Hamani mara moja, ili tupate kufanya lile Esta analoomba.”
Kwa hiyo mfalme na Hamani walihudhuria karamu aliyoiandaa Esta. 6Walipokuwa wakinywa mvinyo mfalme akamuuliza Esta tena, “Sasa haja yako ni nini? Utapewa. Ombi lako ni nini? Hata nusu ya ufalme, utapewa.” 7Esta akajibu, “Haja yangu na ombi langu ni hili: 8Kama mfalme ameona vyema, nami nimepata kibali kwake na kama ikimpendeza mfalme kunipa ombi langu na kunitimizia haja yangu, mfalme na Hamani waje kwangu kesho katika karamu nitakayowaandalia. Kisha nitajibu swali la mfalme.” 9Hamani alitoka siku hiyo kwa furaha na moyo mchangamfu. Lakini alipomwona Mordekai langoni mwa mfalme na kuona kwamba hakusimama wala hakuonyesha hofu mbele yake, alijawa na ghadhabu dhidi ya Mordekai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.