Esta 4:9
Esther 4:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hathaki akarudi kwa Esta na kumwarifu alilolisema Mordekai.
Esther 4:9 in English
Esther 4:9 · Berean Standard Bible
So Hathach went back and relayed Mordecai’s response to Esther.
Context
7Mordekai akamwambia kila kitu ambacho kimempata, pamoja na hesabu kamili ya fedha ambazo Hamani aliahidi kulipa katika hazina ya mfalme kwa ajili ya maangamizi ya Wayahudi. 8Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonyesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake. 9Hathaki akarudi kwa Esta na kumwarifu alilolisema Mordekai. 10Kisha Esta akamwamuru Hathaki amweleze Mordekai, 11“Maafisa wote wa mfalme na watu wa majimbo ya ufalme wanajua kuwa mwanaume au mwanamke yeyote ambaye ataingia kumwona mfalme katika ua wa ndani bila kuitwa, mfalme ana sheria moja tu: Atauawa. Njia pekee kinyume na hili ni mfalme kumnyooshea fimbo ya dhahabu ili aishi. Lakini siku thelathini zimepita tangu nilipoitwa kwenda kwa mfalme.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.