Esta 4:15
Esther 4:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Esta alituma jibu hili kwa Mordekai:
Esther 4:15 in English
Esther 4:15 · Berean Standard Bible
Then Esther sent this reply to Mordecai:
Context
13Mordekai alirudisha jibu hili: “Usifikiri kwamba kwa sababu uko katika nyumba ya mfalme wewe pekee katika Wayahudi wote utapona. 14Kwa kuwa kama utakaa kimya wakati huu, msaada na ukombozi kwa Wayahudi utatoka mahali pengine, lakini wewe na jamaa ya baba yako mtaangamia. Nani ajuaye kwamba hukuja kwenye nafasi ya mamlaka kwa ajili ya wakati kama huu?” 15Kisha Esta alituma jibu hili kwa Mordekai: 16“Nenda, kusanya pamoja Wayahudi wote walioko Shushani, nanyi mfunge kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitakwenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.” 17Kwa hiyo Mordekai alikwenda zake na kutekeleza maagizo yote ya Esta.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.