Native Bible

Ephesians 5:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.”

Ephesians 5:31 in English

Ephesians 5:31 · Berean Standard Bible

“For this reason a man will leave his father and mother and be united to his wife, and the two will become one flesh.”*

Context

29Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza Kanisa lake. 30Sisi tu viungo vya mwili wake. 31“Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” 32Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa. 33Hata hivyo, kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake mwenyewe, naye mke lazima amheshimu mumewe.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.