Waefeso 4:20
Ephesians 4:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo.
Ephesians 4:20 in English
Ephesians 4:20 · Berean Standard Bible
But this is not the way you came to know Christ.
Context
18Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. 19Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kupendelea kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi. 20Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo. 21Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu. 22Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.