Mhubiri 9:13
Ecclesiastes 9:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pia niliona chini ya jua mfano huu wa hekima ambao ulinivutia sana:
Ecclesiastes 9:13 in English
Ecclesiastes 9:13 · Berean Standard Bible
I have also seen this wisdom under the sun, and it was great to me:
Context
11Nimeona kitu kingine tena chini ya jua:
Si wenye mbio washindao mashindano
au wenye nguvu washindao vita,
wala si wenye hekima wapatao chakula
au wenye akili nyingi wapatao mali,
wala wenye elimu wapatao upendeleo,
lakini fursa huwapata wote. 12Zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ajuaye wakati saa yake itakapokuja:
Kama vile samaki wavuliwavyo katika wavu mkatili,
au ndege wanaswavyo kwenye mtego,
vivyo hivyo wanadamu hunaswa na nyakati mbaya
zinazowaangukia bila kutazamia. 13Pia niliona chini ya jua mfano huu wa hekima ambao ulinivutia sana: 14Palikuwa na mji mdogo uliokuwa na watu wachache ndani yake. Mfalme mwenye nguvu akainuka dhidi yake, akauzunguka akaweka jeshi kubwa dhidi yake. 15Katika mji huo kulikuwepo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.