Mhubiri 7:26
Ecclesiastes 7:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nimeona jambo lililo chungu kuliko mauti, mwanamke ambaye ni mtego, ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea na mikono yake ni minyororo. Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa, bali mwenye dhambi atanaswa naye.
Ecclesiastes 7:26 in English
Ecclesiastes 7:26 · Berean Standard Bible
And I find more bitter than death the woman who is a snare, whose heart is a net, and whose hands are chains. The man who pleases God escapes her, but the sinner is ensnared.
Context
24Vyovyote hekima ilivyo,
hekima iko mbali sana na imejificha,
ni nani awezaye kuigundua? 25Nikageuza fikira zangu ili kuelewa,
kuchunguza na kuitafuta hekima
na kusudi la mambo,
na ili kuelewa ujinga wa uovu,
na wazimu wa upumbavu. 26Nimeona jambo lililo chungu kuliko mauti,
mwanamke ambaye ni mtego,
ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea
na mikono yake ni minyororo.
Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa,
bali mwenye dhambi atanaswa naye. 27Mhubiri anasema, “Tazama, hili ndilo nililogundua:
“Nimegundua kitu kimoja baada ya kingine nilipokuwa katika kusudi la mambo: 28ningali natafiti
lakini sipati:
nilimpata mwanaume mmoja mnyofu miongoni mwa elfu,
lakini hakuna mwanamke mmoja mnyofu miongoni mwao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.