Native Bible

Ecclesiastes 7:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yote haya niliyajaribu kwa hekima, nikasema, “Nimeamua kuwa na hekima”: lakini hii ilikuwa nje ya uwezo wangu.

Ecclesiastes 7:23 in English

Ecclesiastes 7:23 · Berean Standard Bible

All this I tested by wisdom, saying, “I resolve to be wise.” But it was beyond me.

Context

21Usitie maanani kila neno linalosemwa na watu, la sivyo, waweza kumsikia mtumishi wako akikulaani: 22kwa kuwa unafahamu moyoni mwako kwamba wewe mwenyewe mara nyingi umewalaani wengine. 23Yote haya niliyajaribu kwa hekima, nikasema, “Nimeamua kuwa na hekima”: lakini hii ilikuwa nje ya uwezo wangu. 24Vyovyote hekima ilivyo, hekima iko mbali sana na imejificha, ni nani awezaye kuigundua? 25Nikageuza fikira zangu ili kuelewa, kuchunguza na kuitafuta hekima na kusudi la mambo, na ili kuelewa ujinga wa uovu, na wazimu wa upumbavu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.