Mhubiri 6:10
Ecclesiastes 6:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lolote lililopo limekwisha kupewa jina, naye mwanadamu alivyo ameshajulikana; hakuna mtu awezaye kushindana na mwenye nguvu kuliko yeye.
Ecclesiastes 6:10 in English
Ecclesiastes 6:10 · Berean Standard Bible
Whatever exists was named long ago, and what happens to a man is foreknown; but he cannot contend with one stronger than he.
Context
8Mtu mwenye hekima ana faida gani
zaidi ya mpumbavu?
Mtu maskini anapata faida gani
kwa kujua jinsi ya kujistahi
mbele ya watu wengine? 9Ni bora kile ambacho jicho linakiona
kuliko hamu isiyotoshelezwa.
Hili nalo ni ubatili,
ni kukimbiza upepo. 10Lolote lililopo limekwisha kupewa jina,
naye mwanadamu alivyo ameshajulikana;
hakuna mtu awezaye kushindana
na mwenye nguvu kuliko yeye. 11Maneno yanavyokuwa mengi,
ndivyo yanavyokosa maana,
Je, hilo linamfaidia vipi yeyote? 12Kwa maana ni nani anayejua lililo jema kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, katika siku chache na za ubatili anazopita kama kivuli? Ni nani awezaye kumwambia yatakayotokea chini ya jua baada ya yeye kuondoka?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.