Mhubiri 3:21
Ecclesiastes 3:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?”
Ecclesiastes 3:21 in English
Ecclesiastes 3:21 · Berean Standard Bible
Who knows if the spirit of man rises upward and the spirit of the animal descends into the earth?
Context
19Hatima ya mwanadamu ni kama ile ya wanyama; wote wana mwisho unaofanana: Jinsi anavyokufa mnyama, ndivyo anavyokufa mwanadamu. Wote wana pumzi inayofanana; mwanadamu hana cha zaidi kuliko mnyama. Kila kitu ni ubatili. 20Wote huenda mahali panapofanana; wote hutoka mavumbini, mavumbini wote hurudi. 21Ni nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?” 22Kwa hiyo nikaona kwamba hakuna kitu kilicho bora zaidi kwa mwanadamu kuliko kuifurahia kazi yake, kwa sababu hilo ndilo fungu lake. Kwa maana ni nani awezaye kumrudisha ili aje kuona kile kitakachotendeka baada yake?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.