Mhubiri 3:20
Ecclesiastes 3:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wote huenda mahali panapofanana; wote hutoka mavumbini, mavumbini wote hurudi.
Ecclesiastes 3:20 in English
Ecclesiastes 3:20 · Berean Standard Bible
All go to one place; all come from dust, and all return to dust.
Context
18Pia nikafikiri, “Kuhusu wanadamu, Mungu huwajaribu ili wajione kwamba wao ni kama wanyama. 19Hatima ya mwanadamu ni kama ile ya wanyama; wote wana mwisho unaofanana: Jinsi anavyokufa mnyama, ndivyo anavyokufa mwanadamu. Wote wana pumzi inayofanana; mwanadamu hana cha zaidi kuliko mnyama. Kila kitu ni ubatili. 20Wote huenda mahali panapofanana; wote hutoka mavumbini, mavumbini wote hurudi. 21Ni nani ajuaye kama roho ya mtu huenda juu na roho ya mnyama hushuka chini ardhini?” 22Kwa hiyo nikaona kwamba hakuna kitu kilicho bora zaidi kwa mwanadamu kuliko kuifurahia kazi yake, kwa sababu hilo ndilo fungu lake. Kwa maana ni nani awezaye kumrudisha ili aje kuona kile kitakachotendeka baada yake?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.