Mhubiri 2:12
Ecclesiastes 2:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha nikageuza mawazo yangu kufikiria hekima, wazimu na upumbavu. Ni nini zaidi mtu anayetawala baada ya mfalme anachoweza kufanya ambacho hakijafanywa?
Ecclesiastes 2:12 in English
Ecclesiastes 2:12 · Berean Standard Bible
Then I turned to consider wisdom and madness and folly; for what more can the king’s successor do than what has already been accomplished?
Context
10Sikujinyima kitu chochote ambacho macho yangu yalikitamani,
hakuna anasa ambayo niliunyima moyo wangu.
Moyo wangu ulifurahia kazi zangu zote,
hii ilikuwa thawabu ya kazi zangu zote. 11Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayo
mikono yangu ilikuwa imefanya
na yale niliyotaabika kukamilisha,
kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbiza upepo;
hapakuwa na faida yoyote chini ya jua. 12Kisha nikageuza mawazo yangu kufikiria hekima,
wazimu na upumbavu.
Ni nini zaidi mtu anayetawala baada ya mfalme
anachoweza kufanya ambacho hakijafanywa? 13Nikaona kuwa hekima ni bora kuliko upumbavu,
kama vile nuru ilivyo bora kuliko giza. 14Mtu mwenye hekima ana macho katika kichwa chake,
lakini mpumbavu anatembea gizani;
lakini nikaja kuona kwamba
wote wawili hatima yao inafanana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.