Mhubiri 11:7
Ecclesiastes 11:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nuru ni tamu, tena inafurahisha macho kuona jua.
Ecclesiastes 11:7 in English
Ecclesiastes 11:7 · Berean Standard Bible
Light is sweet, and it pleases the eyes to see the sun.
Context
5Kama vile usivyofahamu njia ya upepo,
au jinsi mwili uumbwavyo
ndani ya tumbo la mama,
vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu,
Muumba wa vitu vyote. 6Panda mbegu yako asubuhi,
nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee,
kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa,
kwamba ni hii au ni ile,
au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa. 7Nuru ni tamu,
tena inafurahisha macho kuona jua. 8Hata kama mtu ataishi miaka mingi kiasi gani,
na aifurahie yote.
Lakini na akumbuke siku za giza,
kwa maana zitakuwa nyingi.
Kila kitu kitakachokuja ni ubatili. 9Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana,
moyo wako na ukupe furaha
katika siku za ujana wako.
Fuata njia za moyo wako
na chochote macho yako yaonayo,
lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote
Mungu atakuleta hukumuni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.