Mhubiri 1:9
Ecclesiastes 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kile kilichokuwepo kitakuwepo tena, kile kilichofanyika kitafanyika tena, hakuna kilicho kipya chini ya jua.
Ecclesiastes 1:9 in English
Ecclesiastes 1:9 · Berean Standard Bible
What has been will be again, and what has been done will be done again; there is nothing new under the sun.
Context
7Mito yote hutiririka baharini,
hata hivyo bahari kamwe haijai.
Mahali mito inapotoka,
huko hurudi tena. 8Vitu vyote vinachosha,
zaidi kuliko mtu anavyoweza kusema.
Jicho kamwe halitosheki kutazama,
wala sikio halishibi kusikia. 9Kile kilichokuwepo kitakuwepo tena,
kile kilichofanyika kitafanyika tena,
hakuna kilicho kipya chini ya jua. 10Kuna kitu chochote ambacho mtu anaweza kusema,
“Tazama! Kitu hiki ni kipya”?
Kilikuwepo tangu zamani za kale,
kilikuwepo kabla ya wakati wetu. 11Hakuna kumbukumbu ya watu wa zamani,
hata na wale ambao hawajaja bado
hawatakumbukwa
na wale watakaofuata baadaye.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.