Native Bible

Deuteronomy 31:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana atawakabidhi kwenu, nanyi lazima mwatendee yale yote niliyowaamuru.

Deuteronomy 31:5 in English

Deuteronomy 31:5 · Berean Standard Bible

The LORD will deliver them over to you, and you must do to them exactly as I have commanded you.

Context

3Bwana Mungu wenu, yeye mwenyewe atavuka mbele yenu. Ataangamiza mataifa haya mbele yenu, nanyi mtaimiliki nchi yao. Pia Yoshua atavuka mbele yenu, kama Bwana alivyosema. 4Naye Bwana atawafanyia watu hao kile alichowafanyia Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, ambao aliwaangamiza pamoja na nchi yao. 5Bwana atawakabidhi kwenu, nanyi lazima mwatendee yale yote niliyowaamuru. 6Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Bwana Mungu wenu anakwenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi.” 7Kisha Mose akamwita Yoshua na akamwambia mbele ya Israeli wote, “Uwe imara na moyo wa ushujaa, kwa kuwa ni lazima uende na watu hawa katika nchi ile Bwana aliyowaapia baba zao kuwapa, nawe ni lazima uwagawie kama urithi wao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.