Kumbukumbu 31:22
Deuteronomy 31:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hivyo Mose akaandika wimbo huu siku ile na akawafundisha Waisraeli.
Deuteronomy 31:22 in English
Deuteronomy 31:22 · Berean Standard Bible
So that very day Moses wrote down this song and taught it to the Israelites.
Context
20Nitakapokwisha kuwaingiza katika nchi itiririkayo maziwa na asali, nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo, nao watakapokula wakashiba na kufanikiwa, watageukia miungu mingine na kuiabudu, wakinikataa mimi na kuvunja Agano langu. 21Maafa na shida zitakapokuja juu yao, wimbo huu utashuhudia dhidi yao, kwa sababu hautasahauliwa na wazao wao. Ninajua lile wanaloandaa kufanya, hata kabla sijawaingiza katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo.” 22Hivyo Mose akaandika wimbo huu siku ile na akawafundisha Waisraeli. 23Bwana akampa Yoshua mwana wa Nuni agizo hili: “Uwe hodari na shujaa, kwa kuwa utawaleta Waisraeli katika nchi niliyowaahidi kwa kiapo, nami mwenyewe nitakuwa pamoja nawe.” 24Baada ya Mose kumaliza kuandika kwenye kitabu maneno ya sheria hii kutoka mwanzo hadi mwisho,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.