Native Bible

Deuteronomy 30:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo.

Deuteronomy 30:15 in English

Deuteronomy 30:15 · Berean Standard Bible

See, I have set before you today life and goodness, as well as death and disaster.

Context

13Wala hakiko ngʼambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?” 14La hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii. 15Tazama, naweka mbele yako leo uzima na mafanikio, mauti na maangamizo. 16Ninakuamuru leo kwamba umpende Bwana Mungu wako, utembee katika njia zake, na kutunza maagizo yake, amri na sheria zake; ndipo utakapoishi na kuongezeka, naye Bwana Mungu wako atakubariki katika nchi unayoingia kuimiliki. 17Lakini kama moyo wako ukigeukia mbali ukawa huna utii, kama umevutwa kuisujudia miungu mingine na kuiabudu,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.