Kumbukumbu 29:14
Deuteronomy 29:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninafanya Agano hili pamoja na kiapo chake, sio na ninyi tu
Deuteronomy 29:14 in English
Deuteronomy 29:14 · Berean Standard Bible
I am making this covenant and this oath not only with you,
Context
12Mnasimama hapa ili kufanya Agano na Bwana Mungu wenu, Agano ambalo Mungu analifanya nanyi siku hii ya leo na kulitia muhuri kwa kiapo, 13kuwathibitisha ninyi siku hii ya leo kama taifa lake, ili aweze kuwa Mungu wenu kama alivyowaahidi na kama alivyowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo. 14Ninafanya Agano hili pamoja na kiapo chake, sio na ninyi tu 15mnaosimama hapa na sisi leo mbele za Bwana Mungu wetu, bali pia pamoja na wale ambao hawapo hapa leo. 16Ninyi wenyewe mnajua jinsi tulivyoishi nchini Misri na jinsi tulivyopita katikati ya nchi mpaka tukafika hapa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.