Kumbukumbu 25:4
Deuteronomy 25:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Usimfunge maksai kinywa anapopura nafaka.
Deuteronomy 25:4 in English
Deuteronomy 25:4 · Berean Standard Bible
Do not muzzle an ox while it is treading out the grain.*
Context
2Kama mtu mwenye hatia anastahili kuchapwa, mwamuzi atamwamuru alale chini ili achapwe mbele yake idadi ya viboko kulingana na kosa lake, 3lakini kamwe asichapwe zaidi ya viboko arobaini. Ikiwa atachapwa zaidi ya viboko arobaini, nduguyo atadhalilika machoni pako. 4Usimfunge maksai kinywa anapopura nafaka. 5Ikiwa ndugu wanaishi pamoja na mmoja wao akafa bila kuacha mwana, kamwe mjane wake asiolewe nje ya jamaa hiyo. Ndugu wa mumewe atamchukua, amwoe na kutimiza wajibu wa shemeji kwake. 6Mwana wa kwanza atakayemzaa atapewa jina la ndugu aliyekufa ili jina lake lisifutike katika Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.