Native Bible

Deuteronomy 23:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

Deuteronomy 23:17 in English

Deuteronomy 23:17 · Berean Standard Bible

No daughter or son of Israel is to be a shrine prostitute.

Context

15Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake. 16Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimwonee. 17Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. 18Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba ya Bwana Mungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababu Bwana Mungu wako anachukizwa na yote mawili. 19Usimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine chochote ambacho waweza kupata riba juu yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.