Native Bible

Deuteronomy 22:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye,

Deuteronomy 22:23 in English

Deuteronomy 22:23 · Berean Standard Bible

If there is a virgin pledged in marriage to a man, and another man encounters her in the city and sleeps with her,

Context

21huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kufanya ukahaba akiwa nyumbani kwa babaye. Lazima mwondoe uovu katikati yenu. 22Ikiwa mwanaume atakutwa akizini na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanaume na mwanamke aliyezini naye, lazima wauawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli. 23Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye, 24utawachukua wote wawili kwenye lango la mji na kuwapiga kwa mawe mpaka wafe; yule msichana kwa kuwa alikuwa mjini na hakupiga kelele kuomba msaada, na yule mwanaume kwa sababu amemtenda jeuri mke wa mtu mwingine. Lazima mwondoe uovu katikati yenu. 25Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.