Kumbukumbu 21:12
Deuteronomy 21:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mlete nyumbani mwako, anyoe nywele na kukata kucha zake,
Deuteronomy 21:12 in English
Deuteronomy 21:12 · Berean Standard Bible
then you shall bring her into your house. She must shave her head, trim her nails,
Context
10Mkienda vitani kupigana na adui zenu naye Bwana Mungu wenu akawatia adui mikononi mwenu, nanyi mkachukua mateka, 11kama ukiona miongoni mwa mateka mwanamke mzuri wa sura nawe wavutwa naye, waweza kumwoa akawa mke wako. 12Mlete nyumbani mwako, anyoe nywele na kukata kucha zake, 13avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapoweza kumwendea na kuwa mume wake naye atakuwa mke wako. 14Lakini kama hutaendelea kupendezwa naye, mwache aende popote anapotaka. Kamwe huwezi kumuuza au kumtendea kama mtumwa, kwa sababu utakuwa umemvunjia heshima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.