Native Bible

Deuteronomy 20:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi.

Deuteronomy 20:2 in English

Deuteronomy 20:2 · Berean Standard Bible

When you are about to go into battle, the priest is to come forward and address the army,

Context

1Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababu Bwana Mungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi. 2Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi. 3Atasema: “Sikia, ee Israeli, leo unakwenda vitani kupigana na adui zako. Usife moyo wala usiogope, usitishwe wala usitiwe hofu mbele yao. 4Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ndiye huenda pamoja nanyi kuwapigania dhidi ya adui zenu na kuwapatia ushindi.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.