Native Bible

Deuteronomy 2:34 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa wakati ule tuliteka miji yake yote na kuiangamiza kabisa: wanaume, wanawake na watoto. Hatukumwacha yeyote.

Deuteronomy 2:34 in English

Deuteronomy 2:34 · Berean Standard Bible

At that time we captured all his cities and devoted to destruction * the people of every city, including women and children. We left no survivors.

Context

32Wakati Sihoni pamoja na jeshi lake lote walipokuja kukutana nasi katika vita huko Yahazi, 33Bwana Mungu wetu alimweka mikononi mwetu, nasi tukamwangamiza pamoja na wanawe na jeshi lake lote. 34Kwa wakati ule tuliteka miji yake yote na kuiangamiza kabisa: wanaume, wanawake na watoto. Hatukumwacha yeyote. 35Lakini mifugo na nyara tulizoziteka kutoka ile miji tulijichukulia wenyewe. 36Kutoka Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kutoka mji ulio ndani ya bonde, hata mpaka Gileadi, hapakuwa na mji hata mmoja uliokuwa na nguvu kutushinda. Bwana Mungu wetu alitupa yote.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.