Kumbukumbu 2:33
Deuteronomy 2:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana Mungu wetu alimweka mikononi mwetu, nasi tukamwangamiza pamoja na wanawe na jeshi lake lote.
Deuteronomy 2:33 in English
Deuteronomy 2:33 · Berean Standard Bible
And the LORD our God delivered him over to us, and we defeated him and his sons and his whole army.
Context
31Bwana akaniambia, “Tazama, nimeanza kuwapa Mfalme Sihoni na nchi yake kwako. Sasa anzeni kuishinda na kuimiliki nchi yake.” 32Wakati Sihoni pamoja na jeshi lake lote walipokuja kukutana nasi katika vita huko Yahazi, 33Bwana Mungu wetu alimweka mikononi mwetu, nasi tukamwangamiza pamoja na wanawe na jeshi lake lote. 34Kwa wakati ule tuliteka miji yake yote na kuiangamiza kabisa: wanaume, wanawake na watoto. Hatukumwacha yeyote. 35Lakini mifugo na nyara tulizoziteka kutoka ile miji tulijichukulia wenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.