Native Bible

Deuteronomy 12:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mle kama vile mngekula paa na kulungu. Wote walio najisi kiibada na walio safi mwaweza kula.

Deuteronomy 12:22 in English

Deuteronomy 12:22 · Berean Standard Bible

Indeed, you may eat it as you would eat a gazelle or deer; both the ceremonially unclean and the clean may eat it.

Context

20Bwana Mungu wenu atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo. 21Kama mahali ambapo Bwana Mungu wenu atapachagua kuweka Jina lake ni mbali sana kutoka kwenu, unaweza kuchinja wanyama kutoka makundi yenu ya ngʼombe, ya mbuzi na ya kondoo ambayo Bwana amewapa, kama nilivyokuamuru, na mkiwa katika miji yenu wenyewe mnaweza kula nyingi mtakavyo. 22Mle kama vile mngekula paa na kulungu. Wote walio najisi kiibada na walio safi mwaweza kula. 23Lakini hakikisheni kwamba hamkunywa damu, kwa sababu damu ni uhai, kamwe msile uhai pamoja na nyama. 24Hamruhusiwi kamwe kunywa damu; imwageni juu ya ardhi kama maji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.