Danieli 6:21
Daniel 6:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Danieli akajibu, “Ee mfalme, uishi milele!
Daniel 6:21 in English
Daniel 6:21 · Berean Standard Bible
Then Daniel replied, “O king, may you live forever!
Context
19Asubuhi na mapema, mfalme akaondoka na kuharakisha kwenda kwenye tundu la simba. 20Wakati alipokaribia lile tundu, akamwita Danieli kwa sauti ya uchungu, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako unayemtumikia daima, ameweza kukuokoa kwa simba?” 21Danieli akajibu, “Ee mfalme, uishi milele! 22Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lolote baya mbele yako, ee mfalme.” 23Mfalme akafurahi mno, naye akatoa amri Danieli atolewe kutoka kwa lile tundu. Danieli alipotolewa kutoka kwa lile tundu, hakukutwa na jeraha lolote, kwa sababu alikuwa amemtumaini Mungu wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.