Native Bible

Daniel 1:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi akakubali jambo hili, akawajaribu kwa siku kumi.

Daniel 1:14 in English

Daniel 1:14 · Berean Standard Bible

So he consented to this and tested them for ten days.

Context

12“Tafadhali wajaribu watumishi wako kwa siku kumi. Usitupe chochote ila nafaka na mboga za majani* tule, na maji ya kunywa. 13Baadaye ulinganishe sura zetu na vijana wanaokula chakula cha mfalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.” 14Basi akakubali jambo hili, akawajaribu kwa siku kumi. 15Mwisho wa zile siku kumi, walionekana kuwa na afya na kunawiri zaidi kuliko yeyote kati ya wale vijana waliokula chakula cha mfalme. 16Hivyo mlinzi wao akaondoa chakula chao na divai yao waliopangiwa kula na kunywa, akawapa nafaka na mboga za majani badala yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.